Mkuu Mpya wa Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT), Meja Jenerali Samwel Ndomba, akila kiapo mbele ya Rais Jakaya
Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Meja Jenerali Ndomba
anachukua nafasi ya Meja Jenerali Samwel Kitundu, aliyestaafu hivi karibuni kwa
mujibu wa sheria. (Picha na Freddy Maro)
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya
Mrisho Kikwete, akimkabidhi muongozo ya kazi Mkuu mpya wa JKT, Meja Jenerali
Samwel Ndomba, wakati wa hafla ya kumuapisha, iliyofanyika leo asubuhi Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete (kushoto), Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) na Mkuu mpya wa JKT, Meja
Jenerali Samwel Ndomba, wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya hafla
ya kumuapisha Mkuu huyo mpya wa JKT, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange (kushoto) na Mkuu mpya wa JKT, Meja Jenerali Samwel Ndomba, muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment