Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar akutana na wafanyakazi wa Wizara ya Habari
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akifafanua jambo katika mkutano wake na Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo, alipokutana nao leo mjini Zanzibar na kuzungumza, kuhusu masuala mazima ya utendaji kazi zao na matatizo wanayokabiliana nayo, kwenye ukumbi wa Salama Hall, Bwawani Zanzibar. Hii ni baada ya kumaliza kwa ziara yake ya kuzitembelea Idara mbalimbali za Wizara hiyo. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Abdillah Jihad Hassan na kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Bihindi Hamad Khamis. (Picha zote na Yussuf Simai Ali, Maelezo Zanzibar)
Wafanyakazi mbalimbali wa Wizara ya Habari Utamaduni, Utalii na Michezo, wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamadi, alipokutana nao na kuzungumza nao kuhusiana na masuala mazima ya Utendaji wa Kazi zao na matatizo wanayokumbana nayo, ukumbi wa Salama Hall Bwawani Zanzibar.
Baadhi ya w
afanyakazi wa Wizara hiyo, wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shairif Hamadi, alipokutana nao na kuzungumza nao kuhusiana na masuala ya utendaji kazi.
Mfanyakazi wa Kamisheni ya Michezo na Utamaduni, Othman Mohammed (Makombora), akifafanua jambo katika mkutano na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo, mjini Zanzibar leo.
Mfanyakazi wa Kamisheni ya Michezo na Utamaduni, Fatma Issa Juma, akifafanua jambo katika Mkutano na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo, uliofanyika hapo katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Zanzibar.
No comments:
Post a Comment