Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungua watu waliofika
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, kushuhudia ujio wa kombe la
UEFA, jijini Dar es salaam Machi leo 26, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa pamoja na Meneja
Mkuu wa Bia ya Heinken Afrika Mashariki, Koen Morshiu's wakifunua kitambaa,
kuonyesha kombe la Ulaya wakati Kampuni ya bia ya Heinken ambao ndiyo wadhamini
wa kombe la Ulaya (UEFA) walipomkabidhi kombe hilo Waziri Mkuu leo, ofisini
kwake, Kampuni ya Henken pamoja na Shirikisho la mpira wa miguu la ulaya (UEFA)
liko katika ziara ya kulitembeza kombe hilo katika nchi za Afrika na Amerika ya
Kusini, Mexico, Asia nchini China, Tanzania na Kenya.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa pamoja na Meneja
Mkuu wa Bia ya Heinken Afrika Mashariki, KoenMorshiu's wakipiga makofi mara
baada ya kufunua kitambaa kuonyesha Kombe la Ulaya UEFA.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga picha na Kombe hilo
pamoja na Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Mchimbi na
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk Fenella Mukangara (kulia) na Makamu wa kwanza wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu nchini (TFF), Athuman Nyamlani.
No comments:
Post a Comment