TANGAZO


Monday, March 26, 2012

Chama cha ADC chapata usajili wa muda

 Wafuasi wa Chama kipya cha ADC, wakiwa wamepanda pikipiki, Dar es Salaam leo, kumsindikiza Mwenyekiti wao wa Muda, Said Miraj kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya kukabidhiwa Usajili wa muda. (Picha na Dotto Mwaibale)


Wafuasi wa Chama kipya cha ADC, wakipita na ngoma kwenye mtaa wa Samora, jijini Dar es Salaam, kumsindikiza Mwenyekiti wao wa Muda, Said Miraj kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya kukabidhiwa Usajili wa muda leo. (Picha na Dotto Mwaibale)


 Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa (kushoto), akimkabidhi cheti cha usajili wa muda Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Said Miraji katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Msajili, Dar es Salaam leo.



 Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Said Miraji, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukabidhiwa cheti cha Usajili wa Muda wa Chama chake hicho na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, Ofisi ya Msajili, Dar es Salaam.



 Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Said Miraji, akiwa amebebwa juu na wafuasi wake huku akiwa amekinyanyua juu cheti cha usajili wa muda alichokabidhiwa  na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, Ofisi ya Msajili, Dar es Salaam leo.


Wafuasi wa Chama kipya cha ADC, wakisherehekea kupata usajili wa muda kwenye mtaa ya Ohio, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment