TANGAZO


Sunday, March 18, 2012

Wakopti wa Misri waomboleza

Watu wengi wamekesha nje ya kanisa kuu la madhehebu ya Kopti mjini Cairo, kuomboleza kifo cha kiongozi wao, Papa Shenouda wa tatu wa Alexandria.

Papa Shenouda

Alikuwa na umri wa miaka 88.
Papa Shenouda aliongoza madhehebu makubwa kabisa ya Wakristo katika Mashariki ya Kati kwa zaidi ya miaka 40.
Wakopti milioni 10 wa Misri wana siku tatu za kutayarisha maziko yake, na wengi wamepewa ruhusa makazini.
Rambirambi zimekuwa zikitolewa kutoka sehemu mbali mbali za dunia.
Rais Obama alisema Papa Shenouda akitetea uvumilivu na mazungumzo kati ya dini mbali mbali.
Papa Shenouda hakuwa tu kiongozi wa kanisa, lakini piya alihusika sana na siasa.
Mwaka wa 1981 alihitilafiana na Rais Sadat, na akapelekwa uhamishoni; lakini Rais Mubarak alimrejesha.
Chini ya uongozi wake, Wakristo wa Kopti wa Misri wakionekana wanaunga mkono serikali ya Hosni Mubarak, nao wakilindwa dhidi ya Waislamu wa siasa kali.
Atayechukua nafasi yake atakabili kazi ya kuwapa moyo Wakrito wa Kopti, wakati Muslim Brotherhood wanaelekea kushiriki kwa mara ya kwanza, kwenye utawala wa Misri.
Papa Shenouda hakupendelea mabadiliko - chini ya uongozi wake, ilikuwa shida kwa Wakopti waliooana kuweza kuachana.
Sasa Wakopti wengi vijana watataka kiongozi atayewapa mwongozo mwipya katika nchi inayobadilika haraka.

No comments:

Post a Comment