TANGAZO


Tuesday, March 6, 2012

Uturuki yaanza safari za ndege Somalia

Ndege ya shirika la ndege la Uturuki

Shirika la ndege la Uturuki inatarajiwa kuwa shirika la kwanza kuanzisha safari za ndege hadi mjini Mogadisho Somalia.
Naibu wa Waziri mkuu wa Uturuki Bekir Bozdag siku ya Jumanne anatarajiwa kusafiri katika ndege hiyo.
Naibu huyo wa Waziri Mkuu pia amepangiwa kuzindua miradi mbali mbali za maendeleo mjini humo.
Mashirika ya usafiri wa ndege nchini Somalia yamekuwa na safari kati ya Somalia, Djibouti, Kenya na nchi za Kiarabu pekee.
Hii itakuwa safari ya Kwanza kutoka mataifa ya magharibi kuingia Mjini Mogadishu kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa1991 na itakuwa na safari mbili kwa wiki kupitia Khartoum.
Nimezungumza na mbunge Hussein Bantu na kwanza nilimuuliza je Uturuki itaweza kweli kuendesha safari kama hii nchini Somalia.
Shirika hilo la Ndege la Uturuki limepanga kufanya safari mbili kila wiki kati ya Istanbul na Mogadishu.
Hatua hii inakuja wakati baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana mjini New York kujadiliana kuhusu Somalia.
Akizungumza na Idhaa ya Kisomali ya BBC waziri wa Uingereza anayehusika na maswala ya Afrika Henry Bellingham alisema jamii ya kimataifa imeamua kuwa huu ndio wakati muafaka wa Somalia kupata amani na uthabiti wa kudumu.
Waziri huyo ambaye kwa niaba ya Uingereza ,ndiye mwenyekiti wa Baraza hilo katika Mwezi huu wa Machi, amesema mkutano huo ulikubali mapendekezo yote yalioafikiwa katika mkutano wa hivi majuzi wa London kuhusu Somalia.

No comments:

Post a Comment