Viongozi wa wapiganaji na wa makabila katika mji wa Benghazi nchini Libya wamejitangazia utawala wao katika eneo la mashariki mwa nchi kama jimbo lenye uhuru.
Wanasema wanarejea makubaliano ya tangu miaka ya 1950 ya jimbo hilo, likijulikana kama Cyrenaica, lilivyoendeshwa kwa asilimia kubwa ya utawala.Wengi wa watu wa Benghazi wamekuwa wakilalamika kuachwa nyuma na kubaguliwa kwa jimbo lao ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta Hatua hiyo inaleta wasiwasi kwa utawala wa muda mjini Tripoli.
Mwandshi wa BBC Gabriel Gatehouse aliyeko mjini Benghazi katika sherehe hizo amlisema mamia ya watu walikusanyika katika eneo la kuegeshea ndege katika kitongoji kimoja cha jiji la Benghazi.
Walicheza ngoma huku wakitoa kauli za kuunga mkono mfumo wa shirikisho.
Msemaji wa Baraza la wananchi wa Cyrenica aliiambia BBC kwamba makabila na wanajeshi wanaliunga mkono azimio linalohimiza eneo la Mashariki ya Libya lijitawale wenyewe.
Cyrenaica ina utajiri mkubwa wa mafuta na hatua hii itachochea taharuki ya ugomvi katika Tripoli na kwingineko kuwania udhibiti wa mali asili za Libya.
Lakini watu wake wanasema wanachokitaka ni kugawana sawasawa utajiri huo.
Azimio lao halina mashiko ya kisheria .
Kwa sasa Libya iko katika hali ya taharuki za kisiasa lakini baada ya miongo kadhaa ya kutengwa,hatua hii inaungwa mkono na wengi katika mji huu wa pili kwa ukubwa nchini Libya.
No comments:
Post a Comment