Mshambuliaji wa timu ya NSSF ya jijini Dar es salaam, ambao ndio wenyeji wa mashindano ya 9 ya NSSF kwa vyombo vya habari, akihaha kutafuta goli kutoka timu pinzani ya Habari ya Zanzbar wakati wa fainali za mashindano hayo leo jijini Dar es salaam. Timu ya Habari Zanzibar imeibuka kidedea kwa kuifunga NSSF bao 4- 0.
Kocha wa timu ya Habari ya Zanzibar, Taibu Khamis akitoa maelekezo kwa wachezaji wake mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha mchezo wa fainali kati ya timu hiyo na NSSF leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari Vijana na Utamaduni, Dk. Emmanuel Nchimbi, akimkabidhi kombe na Fedha taslimu shilingi milioni 3, nahodha wa timu ya Habari kutoka Zanzibar, Mwanaidi Awadhi, mara baada ya timu hiyo, kuibuka na ushindi kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye mchezo wa mpira wa pete kwa wanawake katika mashindano ya 9 ya NSSF, kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam. Timu hiyo imeifunga timu ya wanawake ya TBC Queens kwa jumla ya magoli 30 kwa 10.
Nahodha wa Timu ya TBC Queens, Grace Kingalame, kombe na zawadi ya mshindi wa pili kwa niaba ya timu yake, shilingi milioni 2, kutoka kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya NSSF kwa vyombo jijini leo.
Nahodha wa timu ya TBC Queens, Grace Kingalame(kulia), akionyesha ujirani mwema kwa kushangilia na wachezaji wa timu ya wanawake ya mpira wa pete ya Habari kutoka Zanzbar licha ya timu hiyo kuifunga TBC Queens magoli 30 kwa 10 katika mchezo wa fainali ya NSSF Cup, jijini leo.
No comments:
Post a Comment