TANGAZO


Tuesday, March 27, 2012

Tibaigana afafanua kuhusu uamuzi wa kusitishwa adhabu ya wachezaji 5 wa Yanga

 Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Tibaigana, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi uliotolewa na kamati yake wa kusitisha adhabu zilizotolewa na Kamati ya Mshindano ya kuwafungia wachezaji watano wa timu ya Yanga, wanaodaiwa kumpiga mwamuzi Israel Nkongo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu hiyo na Azam FC, iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini na Yanga kulala kwa mabao 3-1.  (Picha na Kassim Mbarouk)






 Waandishi na wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari, wakichukua ufafanuzi wa Mwenyekiti huyo, ambaye baadhi ya wadau wa Soka wameanza kumshutumu kutokana na uamuzi huo.





Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Tibaigana, akizungumza wakati akitoa ufafanuzi huo, ambapo alisema kuwa kusitishwa kwa adhabu hiyo sio hukumu ya mwisho bali ni kutaka haki itendeke tu kwani kipo kifungu cha Sheria kinchowapa uwezo huo. Alisema kuwa adhabu iliyotolewa kwa wachezaji hao, ambayo Kamati yake imeisitisha inaweza kuongezwa ikawa kubwa zaidi ama hata kuondolewa kama ikithibitishwa katika ushahidi utakaowasilishwa katika kikao cha Kamati yake. Miongoni mwa wachezaji walihuska katika kadhia hiyo na kupewa adhabu mbalimbali ni Stepheno Mwasyika, Jerryson Tegete,  Nurdin Bakari, Omega Seme na Nadir Haroub 'Cannavaro' . Kulia ni Mwandishi wa Wapo Radio, Mispa Masisi, akichukua maelezo ya ufafanuzi huo. (Picha na Kassim Mbarouk)

No comments:

Post a Comment