Jukwaa la Sanaa lajadili Unenguaji usio na maadili nchini
Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, akisisitiza jambo kwenye Jukwaa la Sanaa, linalofanyika kila wiki Makao Makuu ya baraza hilo, ambapo mada ya wiki hii, ilihusu Sanaa ya Unenguaji na Maleba katika Muziki. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA), Juma Ubao na Mtendaji wa Binti Leo, Betty Kazimbaya. (Picha na Mpigapicha Wetu)
Mwenyekiti wa CHAMUDATA, Juma Ubao, akieleza athari za kuwepo kwa unenguaji usio zingatia maadili kwenye muziki wa dansi, wakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii, Dar es Salaam leo.
Mtendaji kutoka asasi ya Sanaa za Majukwaani ya Binti Leo, Betty Kazimbaya, akiongea na Wadau wa sanaa, kuhusu umuhimu wa Maleba kwa wasanii, wakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa leo jijini. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa hilo, Godfrey Lebejo.
Wadau wa Jukwaa la Sanaa wakifuatilia majadiliano wakati wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment