|
Mkurugenzi wa Kampuni ya Millen Magese, Happines
Magese, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo
Na Mwandishi wetu
WABUNIFU watatu, Doreen Estazia Noni anayetumia Lebo ya eskado bird, Jamila Vera
Swai na Evelyne Rugemalira wamepata nafasi ya kuchaguliwa kwenda kwenye
maonyesho ya mitindo yajulikanayo kama South Africa Fashion Week nchini Afrika
kusini kupitia kampuni ya Millen Magese Group company Limited.
Wabunifu
hao watapanda jukwaani siku ya Aprili Mosi katika onyesho linalobeba jina la
Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX) by Millen Magese introducing
Eskado Bird, Jamila Vera Swai and Evelyne Rugemalira. Millen alipata fursa ya
kutembelea wabunifu hao na kujionea jinsi walivyokuwa wabunifu katika fani hiyo
na kuhamasika kuwachukua na kushiriki katika maonyesho hayo maarufu ya mitindo
katika bara la Afrika.
Alisema
kuwa amevutiwa sana na jinsi walivyokuwa wabunifu na hivyo kuhamasika kuwapa
nafasi hiyo ya kujitangaza kimataifa kwa mara ya kwanza katika historia ya
Tanzania kupitia mradi huu anbao pia dhumuni lake kutangaza vivutio vya utalii
wa Tanzania kimataifa. Alifafanua kuwa mpango huu pia una lengo la kuitangaza
Tanzania kupitia fani ya mitindo dunia nzima kama New York fashion week, London
Fashion Week, Lagos Fashion week na Milan Fashion week.
Alisema
kuwa hayo yanawezekana kutokana na uzoefu wake wa miaka nane katika fani ya
mitindo na mahusiano mazuri kati yake wadau wa mitindo. Mbali ya wabunifu hao,
Millen pia amewapa nafasi wanamitindo watatu, Anastazia Gura (21) na mapacha,
Victoria Casmir (20) na Victor Casmir kuonyesha mitindo katika maonyesho hayo
ya Afrika Kusini.
Wanamitindo
hao wamepata nafasi hiyo baada ya kuwashinda wengine 486 waliofika katika
usaili uliofanyika kwenye hotel ya Serena chini ya majaji, Mustapha Hassanali,
Ritha Poulsen na mwanamitindo maarufu Aminat Ayinde kutoka kampuni ya
America Next top model cycle 12.
Mbali
ya wanamitindo hao Millen pia ameingia mkataba wa kufanya kazi na mwanamitindo
wa kiume, Benard Chizi ambaye pia alishinda katika usaili huo na pia ataungana
na wenzake kwenda Afrika Kusini. Millen pia alionyesha kusikitishwa na
wanamitindo maarufu ambao walikuwa wanawasiliana naye akiwa Afrika Kusini
kutaka kusaidiwa kufika hatua za kimataifa. Alisema kuwa cha kushangaza,
wanamitindo hao, hawajajitokeza katika usaili huo na kumsononesha sana.
“Hii
inaonyesha jinsi gani wanamitindo hao hawajiamini, usaili wangu ulikuwa fursa
pekee ya wao kuonyesha vipaji vyao kimataifa, hata hivyo hawakufika,
nawapongeza waliofika kwani wameonyesha kuwa wanania na ninaamini watafanya
vyema huko Afrika Kusini,” alisema.
|
Mkurugenzi wa Kampuni ya Millen Magese, Happines
Magese (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akiwatambulisha wanamitindo aliowaibua Hoteli ya Serena, hivi karibuni ambao watapanda kwenye
jukwaa la wabunifu wa mavazi na waonesha mitindo nchini Afrika Kusini,
yajulikanayo kama 'South Africa Fashion Week', April Mosi kuonesha vipaji vyao. Kulia ni baadhi ya wabunifu watakwenda nao, nchini humo kuonesha mavazi yao, Evelyn Rugemalila na Doreen Estazia Noni. (Picha na Kassim Mbarouk)
Baadhi ya washiriki ambao wataambatana na Mkurugenzi wa Kampuni ya mitindo ya Millen Magese, Happines
Magese kwenda nchini Afrika Kusini kwenye maonesho ya mavazi na mitindo ya 'South
Afrika Fashion Week', wakionesha mavazi ya wabunifu ambao wataambatana nao pia nchini humo.
Wanamitindo wakiwa wamepozi na mavazi ya wabunifu waendao Afrka Kusini kushiriki Onesho la South Africa Fashion Week
Mmoja wa washiriki waendao Afrika Kusini kwenda kushiriki maonesho ya South Africa Fashion Week, akipozi na moja ya mavazi hayo.
Mwanamitindo akionesha moja ya mavazi yaliyobuniwa na wabunifu waendao kwenye maonesho ya South Africa Fashion Week.
Mwanamitindo Victor Casmir akiwa kwenye pozi na moja ya vazi litakalotumika kwenye maonesho ya Afrika Kusini.
Mwanamitindo, Anastazia Gura, akiwa amepozi na moja ya mavazi yatayotumiwa katika maonesho hayo, nchini Afrika Kusini.
Mbunifu mavazi Evelyn Rugemalila, akionesha waandishi wa habari, baadhi ya mavazi aliyoyabuni na kuchaguliwa kwenda kushiriki kwenye maonesho ya South Africa Fashion Week, nchini humo, Aprili Mosi.
Mmoja wa wanamitindo, aliyeibuliwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Millen Magese, Happiness, walioshinda kwenda Afrika Kusini kushiriki maonesho ya mitindo na mavazi, akipita mbele ya waandishi wa habari, kuonesha kipaji chake kilichompatia nafasi hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye utambulisho wa wabunifu mavazi na waoneshaji mitindo, walishinda kwenda Afrika Kusini kushiriki kwenye maonesho hayo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Millen Magese, Happines
Magese, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, akiwa na
wanamitindo aliowaibua Hoteli ya Serena, hivi karibuni ambao watapanda kwenye
jukwaa la wabunifu wa mavazi na waonesha mitindo nchini Afrika Kusini,
yajulikanayo kama 'South Africa Fashion Week', April Mosi. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Wabunifu mavazi, ambao wamepata nafasi ya kwenda kushiriki kwenye maonesho hayo, wakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Millen Magese, Happiness Magese kwenye utambulisho kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Happiness Magese (katikati), Mkurugenzi wa Makampuni ya Millen Magese, akiwa na kundi la zima la washiriki wa mitindo na wabunifu, ambao ataondoka nao kuelekea Afrika Kusini kwenye maonesho hayo.
Waonesha mitindo Mapacha, walioibuliwa na Happiness Magese (katikati), Mkurugenzi wa Makampuni ya Millen Magese. Victoria Casmir (20) na Victor Casmir wakiwa pamoja naye wakati wa utambulisho huo leo jijini.
Pacha Victor Casmir, akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huo, jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment