TANGAZO


Wednesday, March 28, 2012

AU yafadhaishwa juu ya Sudan na Sudan ya Kusini


Mwanajeshi
Tofauti katika umiliki wa mafuta ni kizuizi kikubwa katika Sudan na Sudan ya Kusini kuelewana
Muungano wa Afrika AU umeelezea wasiwasi kutokana na mapigano ya mpakani kati ya Sudan na Sudan ya Kusini, huku kukiwa na taarifa za mashambulio ya angani yakiendelea.
Hali ya kutoelewana kutokana na mafuta ndio kizuizi kikubwa zaidi kati ya mataifa ya Sudan na Sudan ya Kusini kufikia muwafaka.
Muungano wa Afrika, AU, umeelezea wasiwasi mkubwa kutokana na mapigano yaliyozuka kati ya Sudan na Sudan ya Kusini.
Kufuatia siku mbili za mapigano, mkuu wa AU, Jean Ping, ameyashauri mataifa hayo mawili kuheshimu hatua ya kuwaondoa wanajeshi wao hatua ya kilomita 10 kutoka mpakani.
Ripoti ambazo bado hazijathibitishwa zinaeleza kwamba mapigano yamesitishwa, lakini Sudan iliendelea na mashambulio ya angani katika eneo la Sudan ya Kusini wakati wa usiku.
Mataifa hayo yalipambana vikali na kwa muda mrefu katika, katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, kabla hatimaye Sudan ya Kusini kufanikiwa kujitenga na kuwa taifa huru.
Ghasia ambazo zilianza siku ya Jumatatu hasa zilitokea katika eneo lenye mafuta mengi la Heglig, na vile vile katika eneo Unity, katika Sudan ya Kusini.
Gideon Gatpan, waziri wa habari katika jimbo la Unity, siku ya Jumatano alileleza kwamba ndege za Sudan yalilishambulia eneo ambalo lilikuwa kilomita 35 kutoka mji mkuu wa jimbo la Bentiu, wakati wa usiku, lakini nchi hiyo ilikuwa tayari imesitisha mashambulio yote ya nchi kavu.
Sudan imeamua kuahirisha ziara ya Rais Omar al-Bashir Sudan ya Kusini, ambayo ilitazamiwa wiki ijayo.
Rais huyo alitazamiwa kukutana na mwenzake wa Sudan ya Kusini, Salva Kiir.
Maafisa kutoka mataifa hayo mawili sasa wanatazamiwa kukutana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kwa nia ya kupunguza uhasama kati ya mataifa yao mawili.

No comments:

Post a Comment