Balozi
wa nchi za Umoja wa Ulaya, Filiberto Cerian Sebregondi akizungumza jambo na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile mara baada ya
kumaliza kusaini makubaliano ya msaada wa shilingi bilioni 108, fedha ambazo zimetolewa na
umoja huo kwa ajili ya kuimarisha miradi ya maji katika
mikoa ya Rukwa, Lindi na Kigoma ili kutimiza malengo ya milenia, ifikapo mwaka
2015. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dr. Servacius Likwelile na Balozi wa
nchi za Umoja wa Ulaya nchini, Filiberto Cerian Sebregondi, wakisaini hati za
makubaliano ya msaada wa fedha katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo leo jijini, Dar es
Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 108, zimetolewa na umoja huo, fedha ambazo
zitatumika kuimarisha miradi ya maji katika mikoa ya Rukwa, Lindi
na Kigoma ili kutimiza malengo ya milinia ifikapo mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment