TANGAZO


Thursday, March 15, 2012

Sioi autikisa mji mdogo wa Mbuguni, Arumeru

 Mratibu wa kampeni za CCM Arumeru Mashariki, Mwigulu Nchemba akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano uliofanyika Mbuguni, Kata ya Mbuguni, Arumeru Mshariki leo. (Picha zote na Bashir Nkoromo).



 Mwigulu akimnadi mgombea ubunge wa CCM, Sioi Sumari katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo mji mdogo wa Mbuguni Kata ya Mbuguni, Arumeru Mshariki.


 Mgombea wa CCM, Jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akiomba kura kwa mamia ya wananchi waliohudhutria mkutano wa kampeni za Chama hicho katika mji mdogo wa Mbuguni, Kata ya Mbuguni.


  Baadhi ya wananchi wakicheza ngoma za kundi la TOT kwa ajili ya kumshangilia mgombea wa CCM, Sioi wakati wa mkutano wa kampeni mji mdogo wa Mbuguni Kata ya Mbuguni.


  Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika mji mdogo wa Mbuguni Kata ya Mbuguni, Arumeru.


 Vijana wakimshangilia Sioi kwenye mkutano uliofanyika mji mdogo wa Mbuguni.

 Malikia wa mipasho, Khadija Omari Kopa  na wasanii wenake wa kundi la Tanzania One Thetre (TOT), wakishambulia jukwaa kwenye mkutano wa mji mdogo wa Mbuguni, Arumeru Mashariki.


 Mkurugenzi wa Tanzania One Thetre (TOT), Kapteni John Komba ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, akiimba mbele ya umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni za CCM, mji mdogo wa Mbuguni Jimbo la Arumeru Mashariki.


Mbunge wa Simanjiro mkoani Manyara, Ole Sendeka akizungumza katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment