TANGAZO


Sunday, March 25, 2012

Sioi akiteka kijiji Ngongongare


Mzee mwenye umri wa miaka 120 katika Kijiji cha Ngongongare, Kata ya Maji ya Chai,  Ibrahim Mbise (kushoto) akimuombea baraka kimila mgombea wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, uliofanyika katika kijiji hicho, jana. (Picha na Bashir Nkoromo).




Kinamama wakimshangilia Sioi baada ya msafara wake wa kampeni kuwasili kijiji cha Ngongongare,Maji ya Chai, jana.




Mfuasi wa CCM akishangilia 'kwa raha zake' kwenye mkutano wa kampeni za CCM katika kijiji cha Ngongongare. Kulia ni mmoja wa polisi ambao huwepo kuimarisha ulinzi kila mikutano ya kampeni ya vyama vinavyoshiriki uchaguzimdogo jimboni humo.



Uhaba wa maji katika maeneo kadhaa katika jimbo la Arumeru Mashariki ni miongoni mwa kero ambazo wagombea wa vyama mbalimbali vinavyoshiriki kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo,wamekuwa wakiahidi kuupatia ufumbuzi. Pichani, watoto wakisafiri kwa punda kutafuta maji katika kijiji cha Ngongongare, jimboni humo,jana.

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Ngongongare, Maji ya Chai, akiwa kwenye dirisha la shule hiyo wakati akifuatilia mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho jana.

No comments:

Post a Comment