TANGAZO


Sunday, March 25, 2012

Simba ilivyoinyoa Es Satif Uwanja wa Taifa

Waamuzi wa mchezo wa Kombe la Shirikisho 16 bora, mchezo wa kwanza kati ya Simba ya Tanzania na Es Satif ya Algeria, wakiingia Uwaja wa Taifa, kuchezesha mchezo huo leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Timu ya Simba ikiingia uwanjani, ikiongozwa na nahodha wake, Juma Kaseja.

 


Kikosi cha Es Satif kilichokubali kipigo cha mabao 2-0.
Kikosi cha Simba kilichopambana na Es Satif na kuinyoa mabao 2-0.

 

Wachezaji wa Simba, wakisalimiana na wa Es Satif.


Manahodha wa timu za Simba na Es Satif, wakipiga kura kuchagua upande wa kuanzia.



Waamuzi wakipiga picha ya pamoja na manahodha wa timu hizo.



Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu, akipiga mpira kichwa mbele ya wachezaji wa Es Satif Mokhtari Megueni (20) na Farouk Belkaid.



Amir Maftah wa Simba, akitafuta mbinu ya kumtoka Farouk Belkaid wa Es Satif.

Amir Maftah wa Simba, akijaribu kumpoteza Racid Ferrahi wa Es Satif.



Riadh Benchadi, akiruka pamoja na Patric Mafisango wa Simba, kuupiga mpira kichwa.



Salum Machaku wa Simba, akimpoteza Farouk Belkaid wa Es Satif



Salum Machaku wa Simba, akitafuta mbinu ya kumtoka Mokhtar Begueni wa Es Satif.

Salum Machaku akimpiga chenga Mokhtar Begueni.



Mashabiki wa Simba, wakifuatilia mchezo huo jinsi unavyokwenda.

Mashabiki wa Simba, wakishangilia moja na mabao yaliyofungwa timu hiyo katika mchezo huo.

Mashabiki wa Yanga wakitafakari la kufanya baada ya mambo kuwaendea vibaya timu ya Es Satif
kwa kukubali kipigo kwa Mnyama Simba.

No comments:

Post a Comment