TANGAZO


Sunday, March 4, 2012

Simba yaiondoa Kiyovu mashindanoni

 Waamuzi wa pambano la Kuwania Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Simba na Kiyovu ya Rwanda, wakitoka uwanjani, Uwanja wa Taifa leo jioni, baada ya kupuliza filimbi ya mapunziko kwa timu hizo, ambapo hadi wakati huo, Simba ilikuwa mbele kwa magoli 2-0. (Picha na Kassim Mbarouk)


Godfrey Katerega wa Kiyovu (mbele), akipambana na Emmanuel Okwi wa Simba katika mchezo huo.

 Mchezaji Nassoro Masoud 'Cholo', akidondoka chini huku akivutwa na Julius Bakkabulindi wa Kiyovu katika mchezo huo.


 Mashabiki wa Simba wakiwa na bango lao, wakiishangilia timu yao katika mchezo huo.


 Mashabiki wa Yanga (fulana za njano), wakiwa wameng'oa viti, wakiwafurusha wa Simba, walipovamia jukwa lao wakati wa mchezo huo.


Emmanuel Okwi, mfungaji wa magoli 2 ya Simba, akizungumza na waandishi wa habari baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo huo.

Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, akizungumza na mwamuzi wa mchezo huo, Wush Hagi Yababon, kutoka Somalia baada ya kumalizika kwa kipute hicho, Uwanja wa Taifa, leo jijini.

No comments:

Post a Comment