Maafisa wa uchaguzi wa Urusi wanasema watu wengi wamejitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa rais.
Lakini vyama vya upinzani vinasema visa vingi vya udanganyifu vimetokea.
Maelfu ya watu wanaojitegemea wanasimamia uchaguzi huo na kamera zimewekwa kwenye vituo vya kupigia kura, baada ya tuhuma kwamba kulikuwa na udanganyifu mkubwa kwenye uchaguzi wa wabunge mwezi Disemba, na kupelekea maandamano makubwa kufanywa.
Idadi kubwa ya askari polisi na wanajeshi wako zamu mjini Moscow kuweka nidhamu.
Waziri Mkuu, Vladimir Putin, anagombea urais pamoja na wagombea wengine wane.
Bwana Putin ameshawahi kuwa rais hadi mwaka wa 2008, alitumika mihula miwili kama inavoruhusu katiba
No comments:
Post a Comment