Mchezaji Muganyizi Martin wa Kagera Sugar (kushoto), akijaribu kuutoa mpira miguuni mwa Emanuel Okwi wa Simba, wakati timu zao zilipokutana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Simba ilishinda kwa mabao 3-1. (Picha na Kassim Mbarouk)
Nassor Masoud (Chollo) wa Simba, akipambana na David Charles wa Kagera Sugar katika mchezo huo.
Amir Maftah wa Simba, akijaribu upiga tobo kwa mchezaji Muganyizi Martin wa Kagera Sugar.
Emmanuel Okwi wa Simba, akijaribu kumtoka Freeman Nesta wa Kagera, anayejaribu kuuondoa mpira miguuni mwa Okwi katika mchezo huo.
Wachezaji wa Simba, wakipongezana baada ya Patrick Mafisango, kufunga goli la kwanza la timu hiyo katika mchezo huo, uwanjani hapo leo jioni.
Mchezaji Themi Felix wa Kagera Sugar, akikimbia kushangilia goli alilolifunga la kuusawazishia timu yake, huku golikipa Juma Kaseja wa Simba, akimwangalia, mpira ukiwa umetinga nyavuni kulia kwake na kufanya mpira kuwa bao 1-1 hadi wakati huo.
Wachezaji wa Kagera Sugar, wakishangilia bao lao hilo la pekee katika mchezo wao huo, walioambulia kipigo kitakatifu cha mabao 3-1 hadi mwisho wa mchezo huo.
Nassor Chollo wa Simba (kushoto), akipambana na Themi Felix wa Kagera Sugar.
Mchezaji George Kavilla wa Kagera Sugar, akiuondoa mpira mbele ya Felix Sunzu wa Simba katika mchezo huo.
Felix Sunzu wa Simba, akimtoka beki David Charles (aliyeanguka) wa Kagera Sugar katika mchezo huo.
Shomar Kapombe wa Simba (kushoto), akimtoka David Charles wa Kagera Sugar.
Uhuru Sueiman, akijaribu kumwuliza Emanuel Okwi, aliyeangushwa chini na kupatikana penalti, iliyowapatia goli la pili, lililowekwa kimiani tena na Patrick Mafisango baada ya goli la kwanza kulifunga kwa mkwaju mkali wa adhabu, alioupiga kutoka katikati ya uwanja wa Taifa.
Mashabiki wa Simba wakishangilia goli la tatu la timu hiyo, liliofungwa na Emmanuel Okwi. Hadi mwisho wa mchezo Simba mabao 3 dhidi ya 1 la Kagera Sugar.
No comments:
Post a Comment