Mmoja wa ndugu wa marehemu Samson Mbega, akiwa ameshikilia msalaba, ulioandikwa kumbukumbu ya marehemu Mbega, tarehe ya kuzaliwa na ya kufariki kwake, wakati jenenza lililobeba mwili wake likiondolewa nyumbani kwake, maeneo ya Temeke kwa ajili ya kupelekwa Kanisani kufanyiwa Ibada ya mwisho kabla ya kupelekwa kwao, Kisarawe kwa mazishi, leo Machi 7, 2012. (Picha na Kassim Mbarouk)
Jenenza lililokuwa na mwili wa mwandishi wa habari, Samson Mbega, likitolewa nyumbani kwake Temeke kwa ajili ya kupelekwa kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Temeke kwa ajili ya Ibada na kuagwa.
Gari lililokuwa limebeba mwili wa marehemu Mbega, likiondoka nyumbani kwake, kuelekea Kanisani Temeke.
Baadhi ya waandishi wa magazeti ya Gurdian na Nipashe, alikowahi kufanyia kazi marehemu Mbega, wakielekea Kanisani kwa ajili ya Ibada na Kuagwa kwa mwili wake kabla ya kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Kisarawe kwa mazishi, leo.
Mama wa marehemu Samson Mbega, Catherine Mbega, akisaidiwa kupelekwa kwenye gari kwa ajili ya kwenda Kanisani kwa Ibada ya mwisho na kuagwa mwili wa marehemu huyo.
Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda (kushoto) wa Gazeti la Jambo Leo, hakupitwa na tukio hilo, hapa akiwa na baadhi ya wahariri Mgaya Kingoba (wa pili kushoto), Amir Mhando (kulia), wote wa Habari Leo na Somoe Ngitu wa Nipashe.
Baadhi ya wapwa wa marehemu Mbega, wakiwa nje ya Kanisa la KKKT, Temeke, ulikoagwa mwili wa mjomba wao huyo.
Baadhi ya wanafamilia ya marehemu Samson Mbega, wakiwa Kanisani wakifuatilia Ibada ya wafu, iliyokuwa ikiendeshwa na Mchungaji Jacob Mwangonda wa KKKT, Usharika wa Mabibo, Dar es Salaam.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa marehemu Mbega, wakiwa Kanisani hapo kabla ya mwili kusafirishwa kuelekea Kisarawe kwa mazishi.
Baadhi ya waandishi wa habari, waombolezaji, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Mbega, wakiuaga mwili wa marehemu huyo, kanisani hapo leo mchana.
Akinadada na akinamama, waombolezaji, wakiwa katika msiba huo kanisani hapo.
Baadhi ya waandishi wa habari, ndugu, marafiki na wanafamilia wa marehemu Samson Mbega, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu huyo kanisani hapo.
Mmoja wa mwanamke aliyezaa naye mtoto, akisaidiwa na waombolezaji baada ya kushindwa kujizuia alipokuwa akiuaga mwili wa marehemu Mbega.
Mpigapicha Abeid Butu (kushoto), akimsaidia mmoja wa dada wa marehemu Mbega, Rhoda Mhilu, kanisani hapo.
Shemeji wa marehemu Mbega, mwandishi wa siku nyingi, Julius Mhilu (Macho kumchuzi), nyuma, akijaribu kutoa msaada kwa mmoja wa mtoto wa marehemu Mbega, kanisani hapo.
Mmoja wa wafiwa akiwa amelala kwa kuishiwa nguvu baada ya kuuanga mwili wa marehemu huyo, kanisani hapo leo.
Mmoja wa watoto watatu wa marehemu Mbega, akisaidiwa na jamaa zake wakati wa kuaga mwili wake, kanisani hapo.
Jenenza lilikuwa na mwili wa marehemu Samson Mbega, ukitolewa Kanisani kwa ajili ya kuingizwa kwenye gari kwa safari ya Kisarawe, kwenda kwenda kuzikwa.
No comments:
Post a Comment