Uchumi mkubwa barani Afrika unatarajiwa kuathirika kufuatia maandamano makubwa yatakayoshirikisha mamiya ya wanachama wa mashirika ya wafanyakazi kote nchini Afrika ya kusini, wakipinga kuanzishwa kwa kodi ya barabara pamoja na mpango wa ajira kupitia mikataba ya mda mfupi.
Vyama vya wafanyakazi vya Afrika ya kusini vimekua na migongano na mpango wa serikali wa vituo vinavyotumia mitambo ya electroniki kukusanya pesa kutoka kwa watumiaji wa barabara.Shirika la Cosatu lilitarajia kua maandamano hayo yatahudhuriwa na maelfu ya watu kupinga mfumo huu mpya pamoja na mawakala wa ajira.
Maandamano hayo pia yanalenga kuondoa tabia ya kupanga ajira ambapo mashirika huajiri watu kwa mkataba wa mda mfupi.
Maandamano hayo yaliyoandaliwa na Chama cha wafanyakazi COSATU, ilipangwa kufanyika katika miji 32 kote Afrika kusini.
Chama cha Cosatu kilisema kua kilitarajia hadi watu 100,000 kushiriki maandamano hayo.
Mwandishi wa BBC Milton Nkosi akiwa mjini Johannesburg anasema kua mitaa ya Johannesburg imetanda rangi nyrekundu ya Chama cha COSATU.
Chama hicho kinaonyesha uwezo wake na kuongezea kua ni kukionyesha Chama tawala cha ANC (African National Congress) kua ingawa ni washirika, muungano wa vyama vya ushirika vina uhuru wa kuwaunga mkono wafanyakazi wa Afrika kusini.
"vituo vya kodi ya barabara ni mzigo kwa wananchi wasiojiweza," Alisema katibu mkuu Zwelinzima Vavi.
"tunaiomba serikali na tutakua wazi kwa majadiliano. Tutaitikia wito wa serikali kutafuta suluhu, aliongezea Katibu mkuu huyo.
Serikali imeimarisha barabara kuu zilizokuepo ndani na zilizouzunguka mji wa Johannesburg kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2010.
Inasema kua gharama zilizojitokeza hazikutokana na hisani, na sasa inapanga vituo vyenye mitambo ya electroniki iweze kutumiwa ili kulipia gharama na vilevile kuendelea kuhifadhi ubora wa barabara hizi.
No comments:
Post a Comment