TANGAZO


Thursday, March 22, 2012

SBL Yazindua mradi wa uvunaji maji ya mvua Hospitali ya Wilaya, Iringa


Teddy Mapunda, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya Wilaya ya Iringa mjini kwa ajili ya ujenzi wa matanki katika mradi wa kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya hospitali hiyo na wakazi wa karibu na hospitali hiyo iliyopo Frelimo kata ya Mwangata mjini Iringa.
 

Naibu Waziri wa Maji Injinia Gryason Rwenge, akiweka jiwe la msingi katika hospitali ya Wilaya ya Iringa mjini kwa ajili ya ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji katika mradi wa kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya hospitali hiyo na wakazi wa karibu na hospitali hiyo iliyopo Frelimo kata ya Mwangata mjini Iringa, wanaoshuhudia kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na uwajibikaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Dk. Stella Kiwele Mganga mkuu msaidizi wa hospitali hiyo na Teddy Mapunda mkurugenzi wa Mawasiliano na uhusiano wa (SBL).

Hospitali ambayo mradi wa uvunaji wa maji ya mvu umezinduliwa na wanaoonekana pichani ni baadhi ya wauguzi na wafanyakazi wa hospitali hiyo mara baada ya kuhudhuria uwekaji wa jiwe la msingi.
 

Wafanyakazi wa mradi huo, wakichimba msingi wa kuweka matanki hayo.

No comments:

Post a Comment