Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, akiwa pamoja na Manaibu wake, Julius Mtatiro (katikati) na Isamail Jussa, wakisubiri kumpokea Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Mwembe Yanga kwa ajili ya mkutano wa hadhara. Kulia ni Katibu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama na wafurukutwa wa Chama hicho, wakiwa kwenye mkutano huo, viwanjani hapo jana.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akiwa na Katibu wake Mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad, akiwapungia wanachama wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akiwapungia wanachama na wapenzi wa Chama hicho wakati akiwasili viwanjani hapo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.
Umati wa wanachama, wapenzi na wafurukutwa wa Chama hicho, wakimpungia Mwenyekiti wao, Profesa Lipumba, wakati akiwasili viwanjani hapo.
Mbunge Rukia Kassim (Viti maalum CUF, Chake Pemba), akimtunza fedha msanii wa ngoma ya kibati, Mwalimu Tabu kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, wakati alipokuwa akiburudisha kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba (kushoto), akiwa na Katibu wake Mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad kwenye viwanja hivyo.
Umati wa wanachama, mashabiki na wafurukutwa wa CUF, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka kwenye mkutano huo.
Wanachama wa Chama hicho, wakiimba wimbo wa Chama hicho kabla ya kuanza hutuba za viongozi pamoja na maelezo mbalimbali viwanjani hapo.
Katuga, akikabidhi kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupewa ya CUF na Profesa Ibrahim Lipumba, huku Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali, akifurahia. |
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Zanzibar, Ismail Jussa, akizungumza na kisha kumkaribisha Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Shariff Hamad ili azungumze kwenye mkutano.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, akizungumza kwenye mktano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibarahim Lipumba (kulia), akiwa na Makamu wake, Machano Khamis Ali, wakizungumza jamo kwenye mkutano huo.
Mmoja wa wafuasi wa kundi la Hamad Rashid, ambaye alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi na Mwenyekiti wa Mbeya Mjini, Yasin Mrotwa, akiwaomba radhi wanachama wenzake pamoja na Watanzania kwa kosa alilolifanya na hivyo kuamua kurudi kwenye Chama chake cha CUF.
Katibu Mkuu, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Serkali ya Zanzibar, Maalim Seif Sharifff Hamad, akifurahia kurudi kwa mwanachama huyo.
Umati wa wanachama na wafurukutwa wa Chama hicho, ukipunga mikono, ili kukbaliana na uamuzi wa mwanachama huyo.
Mbunge wa Jimbo la Chonga, Pemba, Haroub Shamis, akifurahia jambo, akiwa pamoja na baadhi a wabunge na baadhi ya viongozi wa chama hicho, kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wanachama na wafurukutwa wa CUF, wakiwa wameweka mikono yao kichwani, ili kuonesha kuathirika na utawala wa Chama kilichopo madarakani sasa (CCM) na kutokukubaliana na hali hiyo, ambapo Naibu Katibu Mkuu wao, Bara, Julius Mtatiro, alikuwa akizungumza nao na kuonesha hali hiyo.
Mbunge wa Lindi Mjini, Barwan, akiwa pamoja na wabunge wenzake, viongozi na wageni mbalimbali kwenye mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa vitengo mbalimbali, Dahlia Maggid (Habari na Mawasiliano) na Abubakar Kitogo (Vijana), wakiwa kwenye mkutano huo.
Mfurukutwa wa CUF, Khadija Mohammed 'Bibi Nganari', akiwa kwenye mkutano huo.
Mfurukutwa wa CUF, Khadija Mohammed 'Bibi Nganari', akiwa amebebwa na mfurukutwa mwenzake, Mohammed Mkingie, kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akihutubia wanacham, wapenzi na wananchi waliofika kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibarhim Lipumba, akihutubia.
Umati wa wanachama, wafurukutwa na wananchi wakipunga mikono ili kukubaliana na hotuba ya Mwenyekiti wao huyo.
Mfurukutwa wa Chama hicho, Mohammed Mkingie, akipita mbio pamoja na watoto wake, Nasra (katikati) na Salum, wakiwa wamebeba bendera za Chama hicho, kwenye mktano huo. |
No comments:
Post a Comment