Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Katibu Mtendaji a
Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango akitoa mada ya ufunguzi wa warsha hiyo
ya siku mbili ya REPOA. Wengine toka shoto Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji
wa REPOA Profesa Samuel Wangwe na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek. (Picha na Ikulu)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha ya siku mbili ya mikakati
ya kiuchumi ya kuondoa umaskini iliyoandaliwa na REPOA katika hoteli ya White
Sands jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dk. Phillip Mpango kwa mada nzuri. Kati yao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA, Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe na Balozi wa Uholanzi nchini Dk. Ad Koekkoek.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Profesa Ibrahim Lipumba baada ya picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe, Balozi wa Uholanzi nchini Dk. Ad Koekkoek, Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dk. Phillip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka hoteli ya White Sands, alikofungua warsha ya siku mbili ya Utafiti.
No comments:
Post a Comment