TANGAZO


Monday, March 5, 2012

Rais Kikwete azindua uhamasishaji kupanda Mlima Kilimanjaro


Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa kupanda Mlima Kilimanjaro, katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro eneo la Marangu, mkoani humo leo
Rais Jakaya Kikwete akihutubia wananchi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa kupanda Mlima Kilimanjaro, kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro eneo la Marangu, mkoani humo.


Rais Jakaya Kikwete, akizungumza muda mfupi kabla ya kumzawadia Jenerali Mirisho Sarakikya (kulia) ambaye kwa umri alionao wa miaka 78, tayari ameshapanda Mlima Kilimanjaro mara 38 na kufika kileleni ambapo pia ana mipango ya kupanda tena, atakapofikisha umri wa miaka 80.



  Rais Jakaya Kikwete akiwa na vijana wapandaji Mlima Kilimanjaro kutoka Botswana.

  Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (aliyeshika fimbo kushoto), Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa, John Hendra (wa tatu kulia), akiungana na wanaume 90 na wanawake 36 kutoka nchi 36 za Afrika, walioanza kupanda Mlima Kilimanjaro leo kwa lengo la kupiga vita unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana.


Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa, John Hendra wakiwa katika uzinduzi wa uhamasishaji kupanda Mlima Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro leo.

No comments:

Post a Comment