TANGAZO


Monday, March 5, 2012

Bonanza la Benki ya Posta (TPB), lafana Hoteli ya Kunduch

 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), wakiwa nje ya Hoteli ya Kunduchi Beach, jana kwa ajili ya bonanza leo, lililofanyika hotelini hapo. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakibadilishana mawazo, huku wakiwasubiri wenzao kwa ajili ya kuanza bonanza leo, lililofunguliwa na Mkurugenzi Mkuu, Sabasaba Moshingi.


 Baadhi ya wafanyakazi wa TPB, wakiwa wamejipumzisha kusubiri ufunguzi wa bonanza hilo.


 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo, wakati alipokuwa akilifungua bonanza la wafanyakazi, Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam jana.

 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuzaji Biashara wa benki hiyo, Andrew Chimazi na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa benki hiyo, Devotha Mhaiki, wakijadilina jambo wakati wa bonanza hilo.


 Baadhi ya wafanyakazi wakifanya mazoezi ya kunyoosha viungo kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali katika bonanza hilo la TPB jana.


 Wafanyakazi wakiendelea na mazoezi ya kuweka viungo vyao katika hali ya kimichezo katika bonanza hilo.


 Mkurugenzi Mkuu, Sabasaba Moshingi (kushoto), akiwa pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki hiyo, wakinyoosha viungo kwa ajili ya matayarisho ya kushiriki michezo mbalimbali kwenye bonanza hilo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa TPB, Grace Nkuzi.



Baadhi ya wafanyakazi wa TPB, wakiwa wamevalia viroba, huku wakipatiwa maelezo jinsi ya kushiriki mbio za gunia, kwenye bonanza hilo.


Baadhi ya wafanyakazi walioshiriki mbio za kufukuza kuku, wakiwa kazini kuwafuata kuku waliotayarishwa kwa shindao hilo.


Mmoja wa wafanyakazi hao, akiliona joto la kufukuza kuku, baada ya kudondoka kutokana na chenga ya kuku huyo, huku mwenzake, akiwa amemuwahi kumshika na hivyo kuwa miliki yake.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria cha TPB, Camir Nkuba, akishindana kwa mbio za gunia na wafanyakazi wa matawi ya benki hiyo katika bonanza hilo.


Timu za wafanyakazi wa TPB, wakishindana katika kucheza mpira wa miguu kwenye bonanza hilo jana.


Mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo, akishiriki katika shindano la upigaji wa mpira kuingiza katika goli dogo mbele yake.


Nao wafanyakazi hawa, hawakuwa nyuma, walikuwa wakishindana katika kulisakata rhumba katika bonanza hilo.


Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuzaji Biashara wa benki hiyo, Andrew Chimazi (kulia), akiwa pamoja na Mameneja Wakuu wa Mambo ya Uhusiano, Noves Moses (katikati) na wa Mikopo midogomidogo, George Mazelengwe, wakifuatilia michezo mbalimbali iliyokuwa ikiendelea kwenye bonanza hilo.


Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kushoto), akibadilishana mawazo na kufurahi pamoja na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu wa benki hiyo, Moses Manyatta (kulia) na Paradise Nkini, wakati wa bonanza hilo jana.


Wafanyakazi nao wakiwa katika mapumziko na kubadilishana mawazo kwenye bonanzo hilo.


Baadhi ya wafanyakazi kutoka kwenye matawi ya benki hiyo, wakibadilishana mawazo huku wakijipumzisha baada ya kushiriki katika michezo mbalimbali ya bonanza hilo.


Hawa nao wakipozi kwa picha, wakati wakijipumzisha kabla ya kuendelea na michezo mingine katika bonanza lao.


Ilikuwa ni wakati wa kujipatia maakuli, baada ya kushiriki katika michezo mbalimbali kwenye bonanza  la TPB, lililofanyika Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam jana.


Mkurugenzi Mkuu, Sabasaba Moshingi, akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali vya benki hiyo, wakijipatia chakula kwenye bonanza hilo, baada ya kushiriki katika michezo mbalimbali.


Baadhi ya wafanyakazi wa matawi ya TPB, wakishindana na wenzao wa Makao Makuu katika mbio za kujiko na kiazi mviringo.


Baadhi ya wafanyakazi wa Makao Makuu waliokuwa wakishindana na wenzao wa matawi katika mbio hizo za vijiko na viazi mviringo kwenye bonanza hilo.


Baadhi ya wafanyakazi wa Makao Makuu wakifuatilia wenzao waliokuwa wakishindana katika mbio hizo.

No comments:

Post a Comment