TANGAZO


Tuesday, March 6, 2012

Rais Kikwete, afungua Mkutano wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwasili Chuo cha Polisi, mjini Moshi leo, Machi 6, 2012, tayari kwa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha na kulia ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema. (Picha na Ikulu)




Rais Jakaya Kikwete, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, Chuo cha Polisi, mjini Moshi leo Machi 6, 2012.




Baadhi ya Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, wakiwa kwenye mkutano huo, wakimsikiliza Rais Kikwete, alipokuwa akiwahutubia, Chuo cha Polisi mjini Moshi.


Rais Jakaya Kikwete akizindua moja ya vitabu vya Muongozi wa Jeshi la Polisi, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, Chuo cha Polisi, mjini Moshi. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha wa kulia kwa Rais ni Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama.


No comments:

Post a Comment