Dk. Bilal, afungua mkutano wa Kimataifa wa kujadili utoaji wa fedha za miradi ya Afya
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kikristo ya Huduma za jamii, Peter Maduki (kushoto), mara baada ya kufungua mkutano wa Kimataifa unaojadili utoaji wa fedha za miradi ya afya kulingana na huduma zinazotolewa katika vituo husika vya afya. Mkutano uliowashirikisha Wahisani na Wajumbe kutoka nchi 15 za Afrika. Katikati ni Waziri wa Afya wa Burundi Dk. Sabine Ntakarutimana. (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutoka Tanzania na baadhi ya viongozi wafadhili wa mkutano huo, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mkutano unaojadili utoaji wa fedha za miradi ya afya kulingana na huduma za afya zinazotolewa kutoka nchi 15 za Afrika wakiendelea na mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa nchi mbalimbali zilizoshiriki mkutano wa Kimataifa unaojadili utoaji wa fedha za miradi ya afya kulingana na huduma zinazotolewa, jijini leo
No comments:
Post a Comment