TANGAZO


Thursday, March 22, 2012

Rais Kikwete afunga maadhimisho ya Wiki ya Maji Iringa

Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika siku ya Maji wakati alipokuwa akiyafunga maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Maji, Uwanja wa Samora, mjini Iringa leo.
 
 
Rais Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya maadhimisho hayo. Katikati ni Meneja wa Miradi endelevu na Uwajibikaji, Nandi Mwiyombela.
 
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda (kulia) na Meneja wa Miradi endelevu na Uwajibikaji, Nandi Mwiyombela, wakiwa wameshikilia vyeti walivyokabidhiwa katika maonyesho wiki hiyo.
 
 
Mtaalam wa Maendeleo ya Jamii katika mradi wa Mazingira wa Ziwa Victoria, Raymond Mariki, akitoa maelezo ya utekelezaji wa majukumu ya mradi huo kwa Rais Jakaya Kikwete katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maji na ufungaji wa Maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Maji, mkoani Iringa leo.
 
 
Rais Jakaya Kikwete, akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa maji Mijini wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Yohana Monjesa katika kilele cha wiki ya maji mkoani Iringa leo.
 
 
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Maji, Vijijini wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Amani Mafuru, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya wiki ya maji mkoani Irinaga leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Grayson Rwenge.
 
 
Rais Jakaya Kikwete akienda kukagua mabanda katika maonesho ya Wiki ya maji yaliyohitimishwa leo, mkoani Iringa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma na kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Grayson Rwenge.

No comments:

Post a Comment