TANGAZO


Thursday, March 22, 2012

Dk.Shein afanya ziara ya Kichama Wilaya ya Magharibi


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la maskani ya Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya, kijiji cha Kama Bondeni, Wilaya ya Magharibi leo katika ziara maalum ya kuimarisha Chama hicho.
Msoma utenzi katika sherehe za Uwekaji wa jiwe la msingi la Maskani ya Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya, Farida Rajab, akighani utenzi wake, uliotoa burudani ndani yake, baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kuweka jiwe la msingi la Maskani hiyo, kijiji cha Kama Bondeni leo, akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama hicho.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea risala  iliyosomwa na Issa Yussuf, wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Maskani hiyo kijijini hapo leo. 
.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi kadi ya CCM, Arafa Jabu Saidi, akiwa ni miongoni mwa wanachama waliokabidhiwa kadi za chama hicho, baada ya kujiunga na chama hicho, wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Maskani ya Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya kijijini Kama Bondeni Wilaya ya Magharibi.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi kadi ya CCM, UWT, Khadija Zeddy Abdallah, akiwa ni miongoni mwa wanachama waliokabidhiwa kadi za Chama hicho, katika hafla hiyo, kijijini hapo.

Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za Chama hicho na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Maskani ya Ari mpya, kasi mpya na Nguvu mpya, kijiji cha Kama Bondeni, Wilaya ya Magharibi leo katika ziara maalum ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi.

No comments:

Post a Comment