Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakishiriki dua maalum ya kumwombea maiti huyo, wakati wa mazishi yake kijijini kwao Bumbwini leo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, akitoa hotuba kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusu utendaji kazi wa marehemu huyo katika chama hicho, enzi za uhai wake.
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (watatu kulia), akiwa katika dua ya mwisho ya kumwombea marehemu mwakilishi huyo, iliyokuwa ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Kaabil, Kulia kwa Rais Shein ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad pamoja na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi na kushoto kwa Rais ni Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd.
No comments:
Post a Comment