TANGAZO


Friday, March 16, 2012

Makamu wa Rais Dk Bilal, azungumza na Ujumbe wa APRM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na ujumbe wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM), wakati ujumbe huo ulipomtembelea Ofisini kwake Ikulu, Dar es Salaam leo, Machi 16, 2012 kwa ajili ya mazungumzo. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)




 Makamu wa Rais  Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na ujumbe huo, ulipokwenda kumuona leo Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo naye.




 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana  na Mjumbe wa  Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM) Tanzania, John Shibuda, baada kumaliza mazungumzo na Ujumbe huo uliofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo.



Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Kiongozi wa jopo la wataalam kutoka Afrika wa ujumbe wa  Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM), Akere Tabeng Muna (kulia) na Mwenyekiti wa Ujumbe huo kutoka Tanzania, Hasa Mlawa (kushoto) baada kumaliza mazungumzo yao ofisini Ikulu jijini Dar es Salaam leo.





Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu na wajumbe wa  Tume ya Wataalamu ya Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika (APRM), baada kumaliza mazungumzo yao, Ikulu jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment