TANGAZO


Friday, March 16, 2012

Mkutano wa kampeni za mgombea wa CCM Kata ya Makiba, watia fora

Wananchi wakimbeba kwa ajili ya kumpeleka jukwaani ili awahutubie, mgombea wao, Sioi Sumari katika mkutano wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliofanyika kijiji cha Makiba, Kata ya Makiba, Arumeru Mashariki jana. (Picha zote na Bashir Nkoromo)



 Sioi akiomba kura kwa wananchi wa Makiba. Kushoto ni Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka  na kulia  ni Mratibu wa kampeni za CCM, Jimbo la Arumeru Mashariki Mwigulu Nchemba.



Katibu wa NEC, Oganaizesheni ya CCM, Asha Abdalla Juma, akihutubia mkutano huo wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa mpira wa kijiji cha Makiba. 





Mbunge wa Mtera, Mjumbea wa NEC ya CCM,  Livingstone Lusinde ' Kibajaji', akiwahutubia wananchi katika mkutano huo, kijiji cha Makiba jana.


 Meja Jenerali mstafu, Mirisho Sarakikya, akizungumza kwa niaba ya wazee katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika Kata ya  Makiba.




 Msanii wa Kundi la sanaa la Tanzania One Theatre (TOT), Hafsa Kazinja, akitumbuiza kwanye mkutano huo, Uwanja wa mpira wa Makiba.




 Mmoja wa mashabiki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Makiba, akishangilia wakati wa mkutano huo.





 Maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo wa kampeni za CCM Kata ya Makiba, wakinyanyua mikono ili kuonesha kumuunga mkono mgombe wa chama hicho, Sioi Sumari.






Mratibu wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mwigulu Nchemba, akizungumza na wananchi pamoja na wanachama walohudhuria kwenye mkutano huo.

No comments:

Post a Comment