Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Selestine Gesimba, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu makubaliano baina ya Serikali na Viongozi wa Taasisi za Kiislamu kuhusu mgogoro wa shule ya Sekondari Ndanda iliyoko Masasi Mkoa wa Mtwara leo, jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine Serikali itawarudisha shuleni mwaka huu wanafunzi wote 62, waliohusika na mgogoro wa shule hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Sheikh Musa Kundecha, Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania na Samweli Kusaga kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Idara ya Sekondari. (Picha na Aron Msigwa - Maelezo)
Viongozi wa Taasisi za Kiislamu Tanzania wakiongozwa na Sheikh Musa Kundecha (wa pili kulia), ambaye ni Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, wakijadili jambo na Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA), Jaafar Mneke (katikati) leo, jijini Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliojadili makubaliano baina ya Serikali na Viongozi wa Taasisi za Kiislamu kuhusu mgogoro wa shule ya Sekondari Ndanda.
Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA), Jaafar Mneke (kulia) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya kusitishwa kwa maandano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kesho, nchini nzima kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kuhusu mgogoro wa shule ya sekondari Ndanda.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ndanda waliosimamishwa masomo kufuatia mgogoro wa shule hiyo wakifuatilia tamko la makubaliano ya viongozi wa dini ya Kiislamu na Serikali lililotolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Selestine Gesimba, kufuatia mkutano wa pamoja uliofanyika tarehe 7 mwezi huu.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndanda, waliosimamishwa masomo yao kufuatia vurugu zilizotokea katika shule hiyo wakitoka ndani ya jengo la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kusomwa makubaliano yaliyowahusisha viongozi wa dini ya Kiislamu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na waandishi wa habari ambapo makubaliano hayo yameeleza kuwa Serikali itawarudisha shuleni wanafunzi wote 62, waliosimamishwa, kuhakikisha kuwa Shule ya Sekondari Ndanda ina mazingira mazuri kwa wanafunzi wa dini zote kitaaluma na kuwawezesha kufanya Ibada zao, shule zote zilizotaifishwa ni miliki ya Serikali kiuendeshaji, ardhi na majengo vyote ni mali ya Serikali na Serikali kufanya utaratibu wa kuwepo vikao na viongozi wa Asasi za dini zote.
No comments:
Post a Comment