Raia mmoja wa Uingereza na mmoja kutoka Italia waliotekwa na watu wenye silaha nchini Nigeria mwaka jana wamefariki kufuatia jaribio la uokozi ambalo halikufanikiwa, ametangaza Waziri Mkuu David Cameron.
Waziri Mkuu amesema kua yumkini Chris McManus - kutoka England ya kaskazini mashariki - na Franco Lamolinara waliuawa na watekaji nyara wao kabla ya shughuli ya uokozi".Vikosi vya Uingereza viliwasaidia wanajeshi wa Nigeria katika operesheni iliyoongozwa na Nigeria, alisema Bw.Cameron.
Watu waliokua na silaha waliwateka nyara wahandisi hao wawili kutoka hoteli waliokua wakiishi huko Birnin Kebbi city, kaskazini magharibi Nigeria,tarehe 12 May, 2011.
Bw. Cameron amesema kua wakuu wa huko waliamua kuendelea na jaribio la kuwaokoa mateka hao baada ya kupokea habari za kuaminika kuhusu mahali walipotelekezwa''
"Fursa ilijitokeza kuweza kuwaokoa. Pia tulikua na sababu ya kuamini kua maisha yao yalikua hatarini''.
Alisema kua 'nasikitika kutangaza kua Bw.McManus a Bw.Lamolinara wamepoteza maisha yao kufuatia operesheni hio.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema kua watekaji nyara wa Bw. McManus na Bw. Lamolinara wamekamatwa.
Serikali ya Uitaliano imesema kua Bw.Cameron alimpigia simu mwenzie wa huko kumpasha habari hizo za kusikitisha.
Bw.McManus na Bw.Lamolinara walikua huko Nigeria kwa ujenzi wa Makao makuu ya Benki kuu ya Nigeria.
No comments:
Post a Comment