Mbunge wa Ilalla, Mussa Azan 'Zungu', akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati 50 kwa Shule ya Msingi Bunge, Dar es Salaam leo. Madawati yaliyotolewa na Mfuko wa Jimbo la Ilala ambayo yalikuwa ni miongoni mwa madawati 303 yaliyogawiwa kwa shule mbalimbali za jimbo hilo. Kulia ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyounge, Christina Wambura.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, wakiwa wameyakalia madawati hayo, mara baada ya Mbunge Mussa Azan 'Zungu' kuyakabidhi madawati hayo. |
Mbunge wa Ilala, Mussa Azan 'Zungu', akiwa amekaa kwenye moja ya madawati 50 aliyoyakabidhi kwa Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Bunge, Christina Wambura (kulia) na mwanafunzi Christophela Francis wa darasa la kwanza, Dar es Salaam leo. Madawati hayo ni sehemu ya madawati 303, yenye thamani ya sh. milioni 22.725, yaliyogawanywa kwa shule mbalimbali za msingi za Jimbo la Ilala, jijini ambayo yametolewa na Mfuko wa Jimbo hilo. (Picha na Kassim Mbarouk)
No comments:
Post a Comment