TANGAZO


Thursday, March 15, 2012

Mama Kikwete mgeni rasmi maadhimisho Siku ya Utepe Mweupe


Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete (wa pili kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Afya na Usatawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda,  leo jijini Dar es Salaam,  kabla ya kuanza matembezi ya kuadhimisha Siku ya Utepe Mweupe Tanzania. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)




 Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete (katikati), akiwa pamoja na Watendaji wengine wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Viongozi wa Taasisi mbalimbali zinazoshughulika na mpango wa uzazi salama na afya ya mama na mtoto, wakishiriki kwenye matembezi ya maadhimisho hayo nchini.  Kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said  Sadick.


Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete, akipatiwa maelezo na Dk. Rose Ntambuto (kulia) wa Taasisi ya  Engender Health, chini ya mradi wa ACQUIRE Tanzania, jijini leo kuhusu shughuli za taasisi hiyo, wakati wa maadhimisho hayo. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)


Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete na Mratibu wa taasisi zinazojishughulisha na mpango wa uzazi salama na afya ya mama na mtoto, Rose Mlay, wakifuatilia shughuli mbalimbali zilizokuwa zikifanyika katika maadhimisho hayo. (Picha na Kassim Mbarouk) 




Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said  Sadick (kushoto), akiwa na Mkurugenzi Mkazi Jeroen van't Pad Bosch wa Taasisi inayojishughulisha na mambo ya ukimwi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation katika maadhimisho hao.


Mwakilishi wa Wabunge wanawake, Mama Magareth Sitta, akizungumza katika maadhimisho hayo.


Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika maadhimisho ya siku hiyo.


Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Utepe Mweupe (White Ribon), Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete, akizungumza na wadau wa afya ya mama na mtoto katika maadhimisho ya siku hiyo.



Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, akionesha kitabu cha Okoa maisha ya mama na mtoto, wakati anakizindua, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo, katika maadhimisho ya Siku ya Utepe Mweupe. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik na kushoto ni Mratibu wa taasisi zinazojishughulisha na uondoaji wa vifo vya mama na mtoto nchini, Rose Mlay. 



Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikuli kitabu cha Okoa maisha ya mama na mtoto, mara baada ya kukizindua, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Utepe Mweupe.




Bendi ya Jeshi la Polisi (Magereza), ikitumbuiza katika maadhimisho hayo.



Waimbaji wa kundi la Mjomba Band, kutoka kushoto, Gwantwa Adam, Ismail Kipira na Aneth Kushaba, wakiimba wimbo unaoitwa Baleanja, wakati kundi hilo lilipotumbuiza katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Utepe Mweupe, Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo. 



Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam, waliohudhuria maadhimisho ya siku hiyo, wakicheza ngoma za Mjomba Band, viwanjani hapo.


Mgeni rasmi katika maadhimishi ya Siku ya Utepe Mweupe, Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete, akiwapungia wadau watu mbalimbali waliokuwepo katika maadhimisho hayo, ili kuwaaga na kisha kuondoka viwanjani hapo.


Baadhi ya wadau wa afya ya mama na mtoto, wakimpungia mgeni rasmi katika maadhimishi ya Siku ya Utepe Mweupe, Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete, wakati akiondoka kwenye viwanja vya maadhimisho hayo.


Kundi la ngoma za asili la Hisia Cultural Troupe la Temeke jijini Dar es Salaam, likitumbuiza katika kilele cha maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment