Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Upanga, Dar es Salaam, Paschazia Kinyondo, akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati 50, yaliyotolewa msaada na Taasisi ya mikopo ya fedha ya Blue Financial Service, Dar es Salaam leo mchana. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo, Shekhar Kanabar, Mwenyekiti wa Kamati ya wazazi ya Shule hiyo, Bruno Marandu (wa pili kulia) na kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Evans Maseke. (Picha na Kassim Mbarouk)
Baadhi ya walimu wa Shule hiyo, wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika hafla hiyo.
Walimu wakimsikiliza Mwalimu Mkuu, Paschazia Kinyondo, wakati alipokuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu Shule hiyo, wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya Walimu na Wajumbe wa Kamati ya wazazi ya shule hiyo, wakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika hafla ya kukabidhi madawati hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya mikopo ya Blue Financial Service, Shekhar Kanabar (wa pili kulia), akimkabidhi moja ya madawati 50, Mwenyekiti wa Kamati ya wazazi ya Shule ya Msingi Upanga, Bruno Marandu, Dar es Salaam jana, ikiwa ni msaada kwa shule hiyo. Wa pili kushoto ni Mwalimu Mkuu Paschazia Kinyondo, Afisa Elimu Vielelezo, Amina Maulid na kulia ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Evans Maseke. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mwalimu Mkuu Paschazia Kinyondo, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya mikopo ya Blue Financial Service, Shekhar Kanabar na Mwenyekiti wa Kamati ya wazazi ya Shule, Bruno Marandu (waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa Elimu Vielelezo, Amina Maulid (kushoto nyuma), Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Evans Maseke na Ofisa Elimu Kata ya Upanga, Anna Shaban, mara baada ya makabidhiano ya msaada huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya wazazi ya Shule, Bruno Marandu (kulia), akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya mikopo ya Blue Financial Service, Shekhar Kanabar kwa msaada huo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule hiyo, wakibeba moja ya madawati hayo, waliyokabidhiwa na Taasisi ya mikopo ya Fedha ya Blue Financial Service kwa ajili ya kuyapeleka madarasani.
No comments:
Post a Comment