Meneja kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru, Arumeru Mashariki, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha CCM, Mwigulu Nchemba (kulia) akimnadi mgombea wa CCM wa jimbo hilo, Sioi Sumari katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, 14/3/2012 katika kijiji cha Shambalai, Kata ya Mbuguni.(Picha na Bashir Nkoromo)
Wananchi wa kijiji cha Shambalai, Kata ya Mbuguni, wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) za uchaguzi mdogo jimboni humo leo.
Mgombea ubunge wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akiwasalimia wanakijiji wakati wa kijiji cha Shambalai Kata ya Mbuguni kabla ya mkutano wa kampeni za CCM leo.
Pamela Sioi akimuombea kura mumewe, mgombea ubunge wa CCM, jimbo la Mashariki, Sioi Sumari kwenye kampeni zilizofanyika kijiji cha Shambalai kata ya Mbuguni, jimboni humo leo.
Mama Sioi (wapili kulia) akishiriki kuserebuka kwa muziki wa hamasa za Chama cha Mapinduzi (CCM), ulioporomoshwa katika kijiji cha Msitu wa Mbogo kata ya Mbuguni kabla ya kuanza kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimboni humo leo.
Sioi Sumari akiwaaga wapigakura wake baada ya kumaliza mkutano katika kijiji cha Msitu wa Mbogo, leo.
"Tupo na ninyi" wanafunzi wa shule ya msingi Msitu wa Mbogo wakisema huku wakionyesha dole gumba msafara wa mgombea ubunge wa CCM Sioi Sumari ulipowasili kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja uliopo jirani na shule hiyo katika kata ya Mbuguni, leo.
No comments:
Post a Comment