TANGAZO


Saturday, March 31, 2012

Makamu wa Rais, Dk. Bilal aweka jiwe la msingi Tawi la CCM, Mwanakwerekwe B, mjini Zanzibar



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifunua pazia ili kuashiria kuweka jiwe la msingi la jengo la Ofisi za tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana,  Machi 30, 2012. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini Magharib, Mohammed Yussuf, wakati alipofika Mkoa huo kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi kwenye la Ofisi za tawi la CCM, Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na mmoja kati ya wazee wa eneo hilo, ambaye ni kati ya wazee waliokuwa na kucheza ‘Chandim’ pamoja. Hapa ilikuwa ni baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye la Ofisi za tawi la CCM, Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

No comments:

Post a Comment