Mhitimu Mathew Shayo, akipokea
cheti cha kuhitimu Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara za
Kimataifa, kutoka Chuo Kikuu cha Biashara za Kimataifa cha India (IIFT), kutoka
kwa Mkurugenzi wa Chuo hicho, Thomas Chako, Dar es Salaam jana. IIFT huendesha kozi hiyo ya MBA-IB kwa ushirikiano na
Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Makamu
Wakuu wa Chuo cha IFM, Profesa Isaya Jairo (wa pili kulia) na Profesa Tadeo
Satta.
Mkurugenzi wa Chuo cha
Biashara za Nje, cha nchini India (IIFT), Thomas Chako akiongea katika mahafali ya
12 ya Shahada ya Uzamili, inayotolewa na Chuo hicho kwa ushirikiano na Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM ) cha Dar es salaam. Chako alikabidhi veti kwa wahitimu
takribani 31. Wengine pichani, kutoka kulia ni Makamu Wakuu wa Chuo cha IFM Prof.
Jairo na Prof. Tadeo Satta na Mkuu wa Chuo hicho Prof. Godwin Mjema. Chako
alihimiza umuhimu wa Tanzania kuzalisha wataalamu wa kutosha wa biashara za
Kimataifa ili kunufaika na fursa za biashara za ulimwengu.
No comments:
Post a Comment