TANGAZO


Sunday, March 4, 2012

Sherehe za Siku ya Wanawake zilivyofana nchini


Mgeni rasmi wa Sherehe ya Siku ya Wanawake nchini, Naibu Waziri wa Wanawake, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalim (kulia), akiwa pamoja na Mbunge wa viti maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Arusha, Catherine Magige (kushoto), wakati wa Sherehe hizo zilizofanyika kwenye hoteli ya Serena, Dar es salaam jana usiku, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, inayotarajiwa kufanyika Machi 8, 2012 duniani kote. Aliyesimama nyuma ni Shamimu Mwasha, mmoja wa wandaaji wa sherehe hizo. (Picha na Mpigapicha Wetu)

Mbunifu wa mitindo ya mavazi, Farha akipita na kivazi chake jukwaani.

Sinta, naye akionesha mavazi yake katika sherehe hizo.

Mmoja wa waoneshaji mitindo ya mavazi akipita na vazi lake la khanga.

Mbunifu wa mitindo ya mavazi, Asia Idarous (kushoto), akiwa pamoja na mbunifu anayetumia nembo ya EVE, wakionesha vazili lililobuniwa na mbunifu huyo.


Shamimu Mwasha (kulia), akiwa na marafiki zake katika sherehe hizo za wanawake.

Shamimu Mwasha (katikati), akiwa na  Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba (kulia) na  Meneja wa mradi wa Mwei Vodacom Tanzania, Mwamvua Mlangwa.

Baadhi ya akinamama waliohudhuria katika sherehe hizo, wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yakitendeka katika hafla hiyo.

Akinamama wakiteta na kufurahia jambo wakati wa sherehe hizo.

 Baadhi ya akinamama waliokuwepo katika hafla ya sherehe hizo, wakifuatilia na wengine kuchukua picha kwa kutumia simu zao, matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka katika hafla hiyo.


Baadhi ya akinamama waliokuwa wamevalia sare za nguo za ubunifu wa mitindo, wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakitendeka katika sherehe hizo.



Akinamama wakifurahia matukio yaliyokuwa yakitendeka katika hafla ya sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment