TANGAZO


Monday, March 26, 2012

Mahafali ya Chuo cha Utumishi wa Umma (IPA), Zanzibar

 Nada Ali Khamis (kushoto), mhitimu wa Diploma ya Rasilimali Watu katika Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar (IPA), akipokea zawadi maalum kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora , Haji Omar Kheri muda mfupi baada ya kuwatunuku wahitimu wa kada mbali mbali katika sherehe za mahafali ya nne ya chuo hicho yaliofanyika katika viwanja vya wizara ya Habari kikwajuni mjini Zanzibar jana. Nada ambaye ni mlemavu wa viungo anajishughulisha na biashara ndogo ndogo. Kulia Mkurugenzi wa IPA, Harusi Masheko. (Picha na Haroub Hussein).




 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheir, akimtunuku zawadi mwanafunzi bora wa Diploma ya Rasilimali Watu katika chuo cha Utumishi wa umma Zanzibar (IPA), Said Mbarouk katika sherehe za mahafali ya nne ya chuo hicho.






 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheir akimtunuku zawadi mwanafunzi bora wa Diploma ya Uongozi wa Umma katika chuo cha utumishi wa umma Zanzibar (IPA), Salha Mansour katika sherehe za mahafali hayo mjini Zanzibar jana.






Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheir akizungumza katika mahafali ya nne ya Chuo hicho.  Kulia Mkurugenzi wa Chuo, Harusi Masheko na Mwenyekiti wa Bodi, Abdalla Suleiman.

1 comment:

  1. mh GOD help us to finish our Diploma programs with full safety and blessing.bless us all amynaaaa

    ReplyDelete