Waziri Mkuu mstaafu Edward, Lowassa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, kabla ya safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo.


Askofu Mkuu mpya wa Jimbo la Ifakara, Muhashamu Salitaris Melchior Libena akiongoza ibada yake ya kwanza akiwa ni Askofu wa Jimbo Jipya la Ifakara baada ya kusimikwa katika sherehe zilizofaanyika jana, Ifakara Morogoro.

Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara, Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa Viongozi wa Serikali waliohudhulia Sherehe hizo za kusimikwa kwake.


Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara, Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa wageni mbali mbali waliohudhulia Sherehe hiyo, wakiwemo waandishi wa habari.


Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo, waliofika kwenye sherehe hizo, ambapo ameliomba Kanisa Katoliki kuisaidia Serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.


Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi akimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa.


Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akisalimiana na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo baada ya kumalizika kwa Sherehe ya Kuzindua Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo iliyofanyika jana Ifakara,Mkoani Morogoro.


Waziri Mkuu mstaafu, Lowassa akibadilishana mawazo na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea.


Waziri Mkuu mstaafu, Lowassa akiwapungia mkono wakazi wa Ifakara, wakati alipokuwa akiondoka katika hafla hiyo.


Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akiwapungia mkono, ili kuwaaga wananchi wakati akiondoka eneo hilo.



Wanafunzi wakitoa burudani ya kumuaga Lowassa.