Mgombea wa nafasi ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sioi Sumari, akisalimiana na wananchi alipowasili kwenye mkutano wa Olkung'wado kata ya Ngarenanyuki jana. (Picha na Bashir Mkoromo)
Wananchi wa kijiji cha Ngabobo wakimthibitishia Meneja wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba kuwa watampa kura mgombea wa chama hicho, Sioi Sumari.
Menaeaja wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba,akiwa amejichanganya na wananchi wa jamii ya Wamasai kwenye mkutano wa Ngabobo, Ngarenanyuki.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira (kushoto), akimnadi mgombea wa Chama hicho, Sioi Sumari kwenye mkutano wa Uwiro, Ngarananyuki.
Elielisia Kaaya wa Uwiro, akibandika kwenye duka lake bango la mgombea Ubunge kupiti CCM, Sioi Sumari ili kuonesha kwamba anamkubali mgombea huyo.
Wazee na kijana wakimsikilizakwa makini mgombea Ubunge kupitia CCM, Sioi Sumari katika mkutano uliofanyika kijiji cha Uwiro, Kata ya Ngarenanyuki.
Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari (kushoto), akizungumza na Mbunge wa Umasaini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, akisalimiana na vijana wa kijiji cha Uwiro, Ngarenanyuki, wakati alipofika hapo kwa ajili ya mkutano wa kampeni zake.
Akianamama wa Ngabobo, wakienda kwenye mkutano wa kampeni wa Sioi Sumari, uliofanyika kijijini hapo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asha Abdallah Juma, akihutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Olkung'wando
Akinamama wa Olkung'wando, Kata ya Ngarenanyuki, wakimshangilia mgombea wa CCM, Sioi Sumari, katika mkutano uliofanyika kijijini hapo.
Mwananchi
akinywa maji kwenye bomba la maji safi, katika kijiji cha Olkung'wado, baada ya
kushikwa na kiu akiwa kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
No comments:
Post a Comment