Basata lawapiga msasa viongozi na wamiliki wa bendi Dar
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Ghonche Materego, akionesha kitabu cha Sera ya Taifa ya Utamaduni kwa viongozi na wamiliki wa bendi za muziki za jijini Dar es Salaam, wakati wa semina iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa wa BASATA,Vivian Shalua. (Picha na Mpigapicha wetu)
Mkurugenzi wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta,' Asha Baraka, akichangia mada kwenye semina hiyo ya viongozi na wamiliki wa Bendi za jijini Dar es Salaam.
Meneja wa bendi ya Mapacha watatu, Khamis Dakota, akizungumzia tatizo la wanenguaji kupandisha nguo zao, mara wanapopandwa na mizuka jukwaani. Pia alishauri vikundi visivyosajiliwa vifuatiliwe.
Meneja wa ukumbi wa maonesho wa Continental wa jijini Dar es Salaam, akielezea hali ya maonesho yanayofanyika ukumbini kwake.
No comments:
Post a Comment