Mchoro wa Jengo jipya la
Ushirika Towers linalojengwa mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, linavyoonekana pichani. (Picha Zote na Richar Mwaikend)
Rais Jakaya Kikwete
akifunua pazia ili kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa jengo hilo linalomilikiwa na
Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC).
Rais Jakaya Kikwete, akikabidhiwa zawadi na
Balozi wa China nchini, wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo hilo
linalojengwa na kampuni ya China.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na baadhi
ya viongozi wa Taasisi za Fedha zilizoikopesha TFC kujenga jengo hilo.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa TFC pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Ushirika Tower.
Wana Ushirika wakiwa na
furaha walipokuwa wakiandamana mbele ya Rais Kikwete wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa jeng la Ushirika Tower na
maadhimisho ya mwaka wa Kimataifa wa Ushirika Duniani, kwenye viwanja vya Mnazi
Mmoja, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washirika wakipita na kupung mikono kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya washirika nchini.
Washirika wakiwa wamenyanyua juu mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa maandamano yao leo.
Baadhi ya wadau na wanaushirika wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete, wakati alipokuwa akiwaahutubia kwenye maadhimisho hayo.
Bendi ya DDC Mlimani
Park, ikitumuiza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ushirika nchini.
No comments:
Post a Comment