TANGAZO


Thursday, March 29, 2012

"Huwezi kupendelewa msimu mzima"

Sir Alex Ferguson
Meneja wa Manchester United anasema huwezi kutegemea klabu kupendelewa na mwamuzi msimu mzima
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amesema hata ikiwa unamtegemea mwamuzi uwanjani kukupendelea ili kufanya vyema, hayo ni mambo ambayo hayawezi kudumu msimu mzima na kukiwezesha klabu kupata ushindi.
Klabu ya Fulham ilimtaka mwamuzi kutoa nafasi ya mkwaju wa penalti ilipokuwa ikilemewa kwa bao 1-0 katika uwanja wa Manchester United wa Old Trafford, mechi ambayo iliiwezesha Man U kuwa mbele ya wapinzani wao, majirani Manchester City, kwa kutangulia kwa pointi tatu.
"Kupendelewa ni hali ambayo hubadilika na haiwezi kudumu kwa msimu mzima," alieleza Ferguson.
"Unapata nafasi ya kupendelewa hapa na pale. Kila klabu hupata hizo nafasi nzuri, na vile vile zile mbaya."
Fulham walihitaji mkwaju wa penalti katika dakika ya 87 siku ya Jumatatu, wakati ilipoonekana dhahiri kwamba Michael Carrick alikuwa amemptega Danny Murphy katika boksi.
Lakini mwamuzi Michael Oliver alitupilia mbali ombi la Fulham, kama alivyokuwa awali amekataa ombi la Manchester United, wakati Stephen Kelly ilielekea aliunawa mpira kutoka kwa Patrice Evra kabla nusu ya kwanza ya mchezo kumalizika.
Afisa wa Manchester City, Patrick Vieira alikuwa amesema siku ya Jumatano kwamba anaamini vilabu vikubwa kama United hupendelewa mara kwa mara, ijapokuwa klabu baadaye kilitoa taarifa kuelezea kwamba matamshi yake yalinukuliwa vibaya.
"Kulingana na alipokuwa amesimama mwamuzi, naelewa kwa nini hakutoa penalti Danny Murphy alipoangushwa. Hii ni kwa kuwa mpira ulikuwa umesogea mahali tofauti kutokana na Michael Carrick kushambulia," Ferguson alieleza.
"Kutoka mahali alipokuwa hakuweza kuona vyema. Ilikuwa ni dai halali."

No comments:

Post a Comment