TANGAZO


Tuesday, March 13, 2012

Dokta Hadji Mponda azindua Mpango Mkakati wa Huduma za Macho nchini

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, akifunua pazia ili kuzindua Mpango Mkakati wa Huduma za Macho nchini, ulioanzia mwaka 2011 hadi 2016, Dar es Salaam leo asubuhi, Machi 13, 2012. (Picha na Kassim Mbarouk)





Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, akifurahia wakati alipokuwa akizindua Mpango Mkakati wa Huduma za Macho, ulioanzia 2011 hadi 2016, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Regina Kikuli na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Donan Mmbando. 




Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda (kulia), akiwa pamoja na wadau wa Sekta ya Afya, wakikionesha kitabu cha Mpango Mkakati wa Huduma za Macho, wakati alipokuwa akizindua Mpango huo, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo. Kauli mbiu ikiwa ni 'Usiache Glaukoma ilete giza kwenye maisha yako. Wa pili kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Regina Kikuli na watatu ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Donan Mmbando.




Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda (kushoto), akimkabidhi kitabu cha Mpango Mkakati wa Huduma za Macho, Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Donan Mmbando, mara baada ya kuzindua Mpango huo, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo asubuhi.



Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda (kushoto), akimkabidhi kitabu cha Mpango Mkakati wa Huduma za Macho, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), Dk. Rufaro Chatora wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam leo, asubuhi.




Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda (kushoto), akimkabidhi kitabu cha Mpango Mkakati wa Huduma za Macho, Mwakilishi wa waandishi wa habari, Zaina Malongo wa Gazeti la Mwananchi.




Wanafunzi wenye ulemavu Mwenywa Shule ya Msingi, Uhuru Mchanganyiko, wakitoka Uwanjani baada ya kutoa burudani ya wimbo wa kwaya katika hafla hiyo.


Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kuzuia Upofu nchini, Daniel Mroso, akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa mpango huo.


Mwakilishi wa Mashirika ya Macho yasiyo ya Kiserikali, Eden Mashayo, akizungumza katika hafla uzinduzi huo.


Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), Dk. Rufaro Chatora, akitoa salamu zake katika uzinduzi wa mpango huo.




Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Regina Kikuli, akizungumza katika uzinduzi huo kabla ya kumkaribisha Waziri wake, kuongea na wananchi pamoja na wadau wa Sekta ya Afya.





Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, akizungumza na wananachi, wageni waalikwa pamoja na wadau wa Sekta ya Afya, wakati alipokuwa akiuzindua Mpango Mkakati wa Taifa wa Huduma za Macho, ulioanzia mwaka 2011 hadi 2016, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo asubuhi, Machi 13, 2012.



Baadhi ya wadau wa Sekta ya Afya, wakimsikiliza Waziri wa Afya, Dk. Hadji Mponda wakati alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo.


Wasanii wa kundi la Seven Blinds, wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo.


Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa mpango mkakati huo, wakifurahia na kupiga makofi, hotuba ya Waziri wa Afya, Hadji Mponda.


Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba), akionesha mfano wa utoaji wa huduma ya macho kwa kumuangalia macho msanii wa kundi lake, Mbagala Omar,  wakati walipokuwa wakitumbuiza kwenye uzinduzi wa mpango mkakati huo.



Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda (katikati), akicheza ngoma za Mjomba Band pamoja na Mkurugenzi wa kundi hilo, Mrisho Mpoto (Mjomba), nyuma yake na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kuzuia Upofu nchini, Daniel Mroso.



Msanii Mrisho Mpoto (kushoto) akiimba sambamba na mwenzake Ismail Kipira, wimbo unaoitwa Macho, wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati huo.




Wananchi na wadau wa Sekta ya Afya wakizirudi ngoma za kundi hilo, wakati wa hafla hiyo.



Baadhi ya wapiga picha wa Televisheni, wakishughulika kutafuta sehemu nzuri ya kuchukua picha zao huku chini yao likiwepo bango la uzinduzi wa Mpango Mkakati huo.

No comments:

Post a Comment