Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (Serengeti Breweries Ltd), Teddy Mapunda akiwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maji, Mhandisi Amani Mafuru, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya maadhimisho ya Wiki ya Maji, mkoani Iringa na Meneja Miradi ya jamii wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella, wakijitayarisha kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kutangaza udhamini na hatua iliyofikiwa ya maandalizi ya wiki hiyo, itakayoadhimishwa Iringa. (Picha na Kassim Mbarouk)
Waandishi wa habari wakiwa katika kipindi cha kuuliza maswali katika mkutano huo, uliofanyika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (Serengeti Breweries Ltd), Teddy Mapunda akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kutangaza udhamini wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji, itakayoadhimishwa mjini Iringa kuanzia Machi 16 na kufikia kilele Machi 22, mwaka huu, pia kuelezea maendeleo ya matayarisho yake. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maji, Mhandisi Amani Mafuru, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya maadhimisho hayo na kulia ni Meneja Miradi ya jamii wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella.
Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maji, Mhandisi Amani Mafuru, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Wiki ya Maji, akielezea kufurahishwa kwake na udhamini wa Kampuni ya Bia ya Serengeti pia hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya maadhimisho hayo. Katikati ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (Serengeti Breweries Ltd), Teddy Mapunda na kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara ya Maji, Nurdin Ndimbe.
Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maji, Mhandisi Amani Mafuru, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Wiki ya Maji, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati alipokuwa akielezea kuhusu kufurahishwa kwake na udhamini wa Kampuni ya Bia ya Serengeti pia hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya maadhimisho hayo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (Serengeti Breweries Ltd), Teddy Mapunda na kulia ni Meneja Miradi ya jamii wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella.
No comments:
Post a Comment